Mpango wa Ubia wa Biashara (Business Partnership Facility-BPF) ulioanzishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubelgiji (DGD) unatoa msaada wa kifedha kwa kampuni kutoka sekta zote zinazochangia katika Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) mfano: kutengeneza nafasi za kazi, kuhifadhi mazingira, kurahisisha upatikanaji wa bidhaa na huduma kwa bei nafuu, ujumuishaji wa wanawake na vijana nk.
BPF hutoa ruzuku bila marejesho ya pesa kati ya euro 50,000 na 200,000 ambayo ni asilimia 50% ya jumla ya uwekezaji.
Kila mwombaji anatakiwa awe na mradi unaoleta pamoja watendaji kutoka sekta binafsi, asasi za kiraia, wasomi au sekta ya umma. Mradi huo lazima uwe sehemu ya ‘biashara kuu’ ya kampuni inayohusika.
Pia waombaji lazima waonyeshe wazi kwamba miradi/mipango iliyowasilishwa inaweza kujitegemea. Mradi huo lazima uwe unafanyika katika ya nchi mmojawapo kati ya: Tanzania, Algeria, Benin, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Côte d’Ivoire, DR Congo, Egypt, Ethiopia, Ghana, Guinea, Kenya, Madagascar, Malawi, Mali, Morocco, Mozambique, Niger, Nigeria, Palestine, Rwanda, Senegal, South Africa, Tunisia, Uganda na Zambia.
Wasilisha maombi kwa kujaza taarifa kwenye linki ifuatayo https://candidate.kbs-frb.be/en/call/2023-I52000-F-A
Dirisha la maombi lilifunguliwa tarehe 1 Agosti 2022. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31 Januari 2023
Kwa maelezo zaidi pitia tovuti: https://www.kbs-frb.be/en/business-partnership-facility-enterprises-sdgs-2023a au wasiliana na:
KBF Contact Center
info@kbs-frb.be
+32 2 500 4 555
KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA ITALY
Read MoreKONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI BERLIN, UJERUMANI 13 ā14 OKTOBA, 2022
Read MoreKONGAMANO YA BIASHARA LA CHINA DAR ES SALAAM TAREHE 26-28 SEPT 20222
Read More