Filters
Regulatory Agencies
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA)
Wakala wa usajili wa biashara na leseni(BRELA) ni shirika la serekali lililo chini ya wizara ya viwanda na biashara. Linahusika na usimamizi wa biashara na sheria zinazohusijka na biashara zikiwemo usajili wa kampuni, usajili wa majina ya biashara,nembo za biashara,hati miliki na vibali vya viwanda. Lilianzishwa kwa sheria ya namba 30 ya mwaka 1997 na lilianza kufanya kazi 3-12-1999.
Read MoreMamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)
Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) ni taasisi ya udhibiti inayofanya kazi chini ya wizara ya fedha iyopewa jukumu la kukusanya mapato yote ya serekali kuu ya jamhuri wa muungano wa Tanzania.Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianzishwa kwa sheria ya Bunge Na.11 ya mwaka 1995,na ilianza kufanya kazi tarehe 1 Julai 1996.
Read MoreMamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)
Mamlaka ya usimamizi wa Mawasiliano Tanzania(TCRA) ni mamlaka ya serikali inayohusika na udhibiti wa sekta za mawasiliano na utangazaji. Imeanzishwa chini ya sheria ya usimamizi wa mawasiliano No.12 ya mwaka 2003 ili kudhibiti mawasiliano ya kielektroniki,huduma za posta na masafa ya mawasiliano.
Read MoreMfuko wa Taifa ya Hifadhi ya Jamii(NSSF)
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ni shirika la serikali linalohusika na ukusanyaji, utunzaji salama, uwekezaji wenye tija na usambazaji wa fedha za kustaafu za wafanyakazi wote katika sekta binafsi za uchumi wa Tanzania ambazo haziko chini ya mifuko ya pensheni ya serikali. Ni mpango wa lazima wa mchango ambao hutoa faida mbalimbali kwa waajiri na wafanyakazi wa sekta binafsi nchini Tanzania.
Read MoreMamlaka ya bandari Tanzania(TPA)
Wakala wa bandari Tanzania(TPA) unaosimamia na kutoa leseni za huduma za bandari nchini. Pia inasimamia uingiaji na utokaji wa meli bandarini na kuhakikisha usalama nchi. Kazi zake kuu kusimamia,kuendeleza na kukuza matumizi ya bandari zinazoihudumia Tanzania na nchii majirani zisizopakana na bandari zikiwemo Malawi, Zimbabwe, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Rwanda na Uganda.
Read MoreShirika la Viwango Tanzania(TBS)
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni taasisi ya Viwango ya Taifa la Tanzania iliyoanzishwa na Serikali kama sehemu ya jitihada ya kuimarisha miundombinu kwa sekta za viwanda na biashara kwenye uchumi nchini. TBS hasa imepewa mamlaka na wajibu wa kuchukua hatua na kudhibiti ubora wa bidhaa za aina mbalimbali na kuhimiza uzingatiaji viwango katika viwanda na biashara.
Read MoreMamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA)
TMDA ina jukumu la kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa dawa na vifaa vya tiba na utambuzi. Jukumu kuu la TMDA limeelezwa katika sera ya Afya, 2007 na mamlaka yake imeainishwa katika sheria ya chakula, dawa na vipodozi Tanzania (TFDCA). Sheria hii inatoa Kanuni bora na ya kina ya udhibiti wa usalama na ubora wa dawa, vifaa tiba na utambuzi tanzania bara. Ili kuboresha utoaji wa huduma kwa umma, TMDA inasimamiwa kama Wakala kwa mujibu wa sheria.
Read MoreWakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi(OSHA)
OSHA ni Wakala wa serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu). Taasisi hii ina wajibu wa kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi vilivyopo katika sehemu za kazi ambavyo vinaweza kusabisha magonjwa na ajali. Wajibu huu unatekelzwa kupitia usimamizi wa Sheria Na. 5 ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.
Read MoreShirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo(SIDO)
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 28 ya Mwaka 1973. Shirika lilipewa majukumu ya kutoa huduma inayolenga kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vidogo vinavyozingatia kuongeza thamani ya raslimali zilizoko nchini; Kuendeleza na kutumia teknolojia rahisi inayopatikana nchini; Kutoa kipaumbele kwa miradi ya uzalishaji inayotumia zaidi nguvu kazi; Kuwezesha utengenezaji wa bidhaa za kutosheleza mahitaji ya wananchi hasa vijijini na ziada kuuza nje ya nchi;
Read More