Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuendelea kuwavutia Wawekezaji kwenye Siku maalum ya Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2020 Dubai ambapo lengo la siku hiyo ni kuitangaza nchi ya Tanzania kwenye Maonesho hayo makubwa Duniani yanayoshirikisha nchi 192.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara tarehe 01 Februari , 2022 Jijini Dar es Salaam wakati akiongoza kikao cha Maandalizi ya Siku ya Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2020 Dubai kilichoshirikisha viongozi wa Taasisi za Serikali na Sekta Bianfsi.
Prof. Godius Kahyarara amesema kuwa Siku ya hiyo inalenga kutangaza miradi mikubwa ya uwekezaji hivyo amezitaka Taasisi zinazoshiriki kwenye Siku hiyo kuhakikisha zinakuwa na taarifa kutosha za miradi ili kuwashawishi wakezaji kuwekeza nchini.
Prof. Kahyarara ameongeza kuwa sisi kama waandaaji tunapaswa kuwa na taarifa za kutosha na za kina za fursa za uwekezaji zilizopo nchini ili kupata wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania na sio kutoa taarifa ambayo haijitoshelezi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa Khamis ambao ndio waratibu wa ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho hayo alieleza kuwa kwenye Maonesho ya EXPO 2020 Dubai kila Nchi inapewa fursa ya kuandaa Siku ya Kitaifa kwenye Maonesho hayo ili kujitangaza ambapo siku maalum ya Tanzania itakuwa tarehe 26 Februari, 2022 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Bi. Latifa ameongeza kuwa kwenye siku hiyo mgeni Rasmi anatarajiwa kutembelea Banda la Tanzania, Banda la Wanawake (Women Pavilion) pamoja na banda la “ Nature Pavilion “ na siku hiyo itapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Tanzania na anatarajiwa kuhudhuria kwenye Kongamano la Biashara na Uwekezaji linalotarajiwa kufanyika siku ya Tarehe 27 Februari, 2022 ambapo, atahutubia na kushuhudia utiaji wa saini wa mikataba ya Biashara na Uwekezaji kwenye Kongamano hilo.
DC Jokate Mwegelo Azindua Rasmi Tuzo Za Wajasiriamali Wa Twcc Jijini Dar
Read MoreTaarifa Kwa Mawakala Na Waagizaji Wa Bidhaa Za Chakula Na Vipodozi Nje Ya Nchi
Read MoreWaziri Bashe Atangaza Sikukuu Ya Wakulima Nane Nane Kufanyika Mwaka Huu Wa 2022
Read More