Waziri wa Kilimo Hussein Bashe leo tarehe 29 Januari, 2022 ametangaza rasmi kurejea kwa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi maarufu kama Nane Nane kwa mwaka 2022.
Waziri Bashe amesema baada ya timu ya Wizara kupitia na kubuni namna bora kulingana na mazingira ya sasa ya namna bora ya kuendesha maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mambo kadhaa yamefanyiwa maboresho na kushauri namna bora ya kuendesha maonesho hayo yenye zaidi ya miaka 27 tangu kuanzishwa kwake.
Waziri Bashe amesema jambo la kwanza ni kuyaendesha maonesho hayo ili kuwa endelevu; Kwa kuanzisha Vituo vya mafunzo kwa Wakulima msimu wote wa mwaka na wakati huo Vituo hivyo kuwa atamizi (Incubate) kwa Wakulima kwa kutumia teknolojia mbalimbali za kilimo kwa kipindi chote cha mwaka.
Waziri Bashe ameongeza kuwa hivi karibu Wizara kwa kushirikiana na Serikali za mikoa itautangaza mkoa mwenyeji wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane kwa mwaka huu wa 2022.
Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) kwa mwaka 2021 hayakufanyika; Yalihairishwa kwa tangazo la Waziri wa Kilimo wa wakati huo Prof. Adolf Mkenda; Tangazo alilitoa tarehe 10 Februari, 2021 Jijini Dodoma ambapo ilielezwa kuwa Serikali inafanya tathmini ya namna bora ya kuyaendesha maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) kwa namna bora.
Maadhimisho ya Nane Nane yalianza rasmi mwaka 1994 na yamekuwa yakiadhimishwa katika Kanda Nane kama ifuatavyo: - Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, uwanja vya John Mwakangale, Uyole, Jjijini Mbeya; Kanda ya Kaskazini, uwanja wa Themi, Jijini Arusha; Kanda ya Mashariki, uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Manispaa ya Morogoro; Kanda ya Ziwa, uwanja wa Nyamhongolo, Jijini Mwanza; Kanda ya Kati, Uwanja wa Nzuguni katika Jiji la Dodoma; Kanda ya Magharibi, Mkoani Tabora katika uwanja wa Ipuli; Kanda ya Ziwa Viktoria Mashariki, Mkoa wa Simiyu katika uwanja wa Nyakabindi na mwisho ni Kanda ya Kusini..
DC Jokate Mwegelo Azindua Rasmi Tuzo Za Wajasiriamali Wa Twcc Jijini Dar
Read MoreTaarifa Kwa Mawakala Na Waagizaji Wa Bidhaa Za Chakula Na Vipodozi Nje Ya Nchi
Read MoreRaisi Samia Kuwa Mgeni Rasmi Siku Ya Maalum Ya Tanzania Kwenye Maonyesho Ya Expo Dubai 2020
Read More