Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amewataka wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika Majukwaa mbalimbali hapa nchini.
DC Mwegelo ameyasema hayo leo Januari 29,2022 akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla kwenye uzinduzi rasmi wa tuzo za Wafanyabiashara wanawake Wenye Viwanda zinazo andaliwa na Chama Cha wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC) zinazotolewa Machi 8 Mwaka huu katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa kila mwaka Duniani kote.
Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi mahili wa Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawake wanapata fursa za kumiliki uchumi wao na kuwa na majukwaa mbalimbali yanayotumika kutoa Elimu, mitaji na fursa za masoko ndani na nje ya nchi.
"Serikali yetu chini ya uongozi wa Rais wetu mpendwa Mama yetu Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa mchango mkubwa kwa makundi mbalimbali ya wanawake kuweza kumiliki uchumi wake, hivyo ni wakati wa wanawake kuthamini, kujipanga na kusonga mbele" amesema Jokate.
Amewataka wafanyabiashara kujitokeza kushiriki katika tuzo hizo kwa kujiandikisha kwa wingi kuanzia leo Januari 29,2022 baada ya kuzinduliwa.
Awali akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa TWCC Taifa Mercy Silla amemshukuru Rais Samia kwa kuwezesha majukwaa mbalimbali ya wanawake nchi na kwamba kuwepo kwa majukwaa hayo yameipa fursa Taasisi hiyo kukutana na wanawake wengi katika Mikoa yote hapa nchini.
"Tunamshukuru sana Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuturudishia majukwaa yetu ya wanawake na yeye mwenye analisimamia hili, kwakweli tumeanza kuona mwanga" amesema Mercy Silla.
Nae Mkurugenzi wa TWCC Mwajuma Hamza amemshukuru DC Jokate Mwegeleo kufika kwenye hafla hiyo na kwamba ujio wake umeleta faraja kubwa kwa wanachama wao.
Taarifa Kwa Mawakala Na Waagizaji Wa Bidhaa Za Chakula Na Vipodozi Nje Ya Nchi
Read MoreWaziri Bashe Atangaza Sikukuu Ya Wakulima Nane Nane Kufanyika Mwaka Huu Wa 2022
Read MoreRaisi Samia Kuwa Mgeni Rasmi Siku Ya Maalum Ya Tanzania Kwenye Maonyesho Ya Expo Dubai 2020
Read More