Tanzania News

FURSA YA MAFUNZO NA MITAJI KUTOKA STANBIC BANK

Je, wewe ni mwanamke unayefanya ujasiriamali au biashara ndogo katika kusindikaji  na kuongeza thamani ya vyakula vitokanavyo na mboga mboga, matunda, nafaka na mwani? Na je unafanya shughuli zako kwenye mpaka wa Horohoro,  Namanga, Holili Kasumulu au  Tunduma na una hamu ya kuinua biashara yako kufikia viwango vipya? Tuna fursa ya kusisimua kwako.

Stanbic Biashara Incubator kupitia mradi wa 'Cross Border Program', kwa kushirikiana na Foundation for Civil Society kwa kupitia mradi wa 'Civil Society for Inclusive and Consumer-Centric Trade in Tanzania’ unaofadhiliwa na TradeMark africa, ndiyo njia yako ya kujengewa uwezo, kupanua masoko yako, na kuunganishwa na mitaji na mikopo. Programu hizi mbili zitakuunganisha na jamii ya wapambanaji na itakupa zana, wataalamu na msaada unaohitajika ili kufanikiwa katika sekta yako.

Kupitia ushirikiano huu, Stanbic Bank Biashara Incubator na Foundation for Civil Society watatoa mafunzo, ushauri na uelekezaji maalum kuhusu maandalizi ya kuuza bidhaa nje ya nchi, upatikanaji wa fedha za biashara, upatikanaji wa masoko, na kuongeza thamani katika bidhaa na huduma. Mpango huu pia utahimiza usawa wa kijinsia na ujumuishaji wa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, kuhakikisha kuwa wajasiriamali hawa wanapata fursa za kuboresha maendeleo ya biashara zao. Makubaliano haya yanakusudia kuunda mazingira wezeshi ya biashara kwa kuboresha upatikanaji wa fedha, kujenga uwezo, na huduma maalum za maendeleo ya biashara kwa wajasiriamali wadogo na wa kati. Mpango huu unalingana na juhudi za kuhamasisha ujasiriamali, kukuza uchumi, na kuongeza fursa za ajira nchini Tanzania.

Tuma maombi kupitia link hii  yako kabla ya tarehe ya mwisho ya 13 Machi 2025.

Related Articles

Tanzania News | 07-02-2022

DC Jokate Mwegelo Azindua Rasmi Tuzo Za Wajasiriamali Wa Twcc Jijini Dar

Read More
Tanzania News | 07-02-2022

Taarifa Kwa Mawakala Na Waagizaji Wa Bidhaa Za Chakula Na Vipodozi Nje Ya Nchi

Read More
Tanzania News | 07-02-2022

Waziri Bashe Atangaza Sikukuu Ya Wakulima Nane Nane Kufanyika Mwaka Huu Wa 2022

Read More