Tanzania News

TANGAZO LA NAFASI 8,000 ZA MAFUNZO YA UFUNDI STADI YALIFADHILIWA NA SEREKALI KWA 100%

  1. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inatekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini inayolenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira. Ofisi imeingia makubaliano na vyuo 52 vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi ambavyo vimesajiliwa na Mamlaka husika kutoa mafunzo katika fani mbalimbali zikijumuisha ubunifu wa Mitindo na Ushonaji Nguo, Ufundi Bomba, Uashi, Useremala, Uchomeleaji na uungaji vyuma, Upakaji rangi na maandishi ya alama, Upishi, Utengenezaji wa vipuri vya mitambo, Ufundi Magari na Mitambo, Umeme wa majumbani na viwandani, Umeme wa Magari, Huduma za Hoteli na Utalii, Ukataji Madini na Ufundi vyuma.
  2. Ofisi inawatangazia vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo katika mojawapo ya fani zilizoorodheshwa hapo chini wafike katika vyuo vya VETA vya Mikoa na Wilaya pamoja na vyuo vilivyoainishwa hapa chini ili kuchukua fomu ya kuomba kujiunga na mafunzo. Serikali itafadhili ada ya mafunzo kwa asilimia 100. Mwanafunzi/mzazi/mlezi atagharamia gharama nyingine zikijumuisha nauli ya kwenda chuoni na kurudi nyumbani. Mafunzo yataanza tarehe 03 Machi, 2025 na yatakuwa ya kutwa. Mwombaji anashauriwa kuomba mafunzo haya katika chuo kilicho katika Mkoa anaoishi.
  3. Vituo vilivyokubalika na Serikali kutoa mafunzo hayo na fani zake vimeambatishwa.
  4. Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 31 Januari, 2025 hadi 12 Februari, 2025 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:

               i. Barua ya maombi ya mafunzo;

               ii. Nakala ya Cheti cha kuzaliwa;

               iii. Nakala ya Cheti cha elimu uliyohitimu;

                 iv. Kitambulisho cha uraia/kadi ya mpiga kura (Kwa wenye miaka 18 na   kuendelea);

              v. Barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji anakoishi mwombaji; na

            vi. Picha nne za paspoti (ziandikwe majina matatu ya mwombaji kwa nyuma).

Sifa za kujiunga na mafunzo haya ni:

i. Elimu ya msingi au zaidi kwa fani za ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo, ufundi bomba, ujenzi, useremala, uchomeleaji na uungaji vyuma, upakaji rangi na maandishi ya alama;

ii. Elimu ya kidato cha nne na kuendelea kwa fani nyingine zilizobaki zikijumuisha fani ya utengenezaji wa vipuri vya mitambo, ufundi magari, umeme wa majumbani na viwandani, umeme wa magari na umeme wa jua (solar);

iii. Awe Mtanzania; iv. Awe na umri kati ya miaka 15 – 35; na v. Awe mwenye afya njema.

iii.Vijana Wenye Ulemavu wanasisitizwa kuomba fursa hizi na watapewa kipaumbele katika nafasi za mafunzo haya;

iv.Maombi yachukuliwe na kuwasilishwa kwenye vyuo vilivyo katika mkoa wako ambavyo vimekubaliwa na Serikali kutoa mafunzo haya.

v.Watakaokidhi vigezo na sifa tu ndio watakaochaguliwa..

vi.Tangazo hili linapatikana katika Tovuti ya Ofisi (www.kazi.go.tz)

NB: Fomu za maombi zinapatikana katika vyuo vyote vilivyopitishwa na Serikali kutoa mafunzo haya.

BONYEZA HAPA KUPATA ORODHA YA VYUO VILIVYOKUBALIWA NA SERIKALI KUTOA MAFUNZO

Related Articles

Tanzania News | 07-02-2022

DC Jokate Mwegelo Azindua Rasmi Tuzo Za Wajasiriamali Wa Twcc Jijini Dar

Read More
Tanzania News | 07-02-2022

Taarifa Kwa Mawakala Na Waagizaji Wa Bidhaa Za Chakula Na Vipodozi Nje Ya Nchi

Read More
Tanzania News | 07-02-2022

Waziri Bashe Atangaza Sikukuu Ya Wakulima Nane Nane Kufanyika Mwaka Huu Wa 2022

Read More