Tanzania Women Chamber of Commerce

KONGAMANO LA KUWAANDAA WANAWAKE NA FURSA ZA UWEKEZAJI NA MASOKO

Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) imeandaa kongamano maalum kwa wanawake na vijana lenye lengo la kuwaandaa kwa fursa za uwekezaji na masoko mwaka 2025. Kongamano hili litafanyika tarehe 5 Februari 2025, katika Hyatt Regency Hotel, Dar es Salaam, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Kauli mbiu ya kongamano: “2025: Mwaka Mpya, Mwaka Wako.”

Kongamano hili limepangwa kuwapa wanawake na vijana maarifa na mbinu bora za kujiimarisha kibiashara, kutumia masoko mtandao, na kuchangamkia fursa za soko huru la Afrika (AfCFTA).

Agenda Kuu za Kongamano:

  1. Kujenga mtandao wa kibiashara (Networking).
  2. Mbinu za kukuza na kuendeleza masoko.
  3. Fursa kwa wanawake na vijana katika soko huru la Afrika (AfCFTA).
  4. Kuchochea ubunifu wa vijana katika biashara.
  5. Jinsi ya kutumia masoko ya mtandaoni kutangaza na kuuza bidhaa.
  6. Fursa za biashara na uwekezaji kwa mwaka 2025.

Gharama na Malipo:
Gharama ya ushiriki ni TZS 30,000. Malipo yanaweza kufanywa kupitia:

  • Vodacom Lipa Namba: 5559999 (Jina: Tanzania Women Chamber of Commerce)
  • M-Pesa Namba: 0757823982 (Jina: Tanzania Women Chamber of Commerce)

Washiriki wanahimizwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 3 Februari 2025.

Walengwa:
Wanawake na vijana wanaopenda kuchangamkia fursa za biashara na uwekezaji. Nafasi ni chache, hivyo wahi mapema!

Kwa maelezo zaidi:
Piga simu kwa: 0757823982.

Kongamano hili ni fursa adhimu ya kupanua mtazamo wa kibiashara na kujiimarisha kwa mwaka mpya. Usikose!

Related Articles

Tanzania Women Chamber of Commerce | 12-07-2022

RAIS MWINYI AWAPONGEZA WAJASIRIAMALI WA TWCC

Read More
Tanzania Women Chamber of Commerce | 11-09-2022

TWCC WOMEN IN BUSINESS BREAKFAST MEETING 10 SEPTEMBA 2022

Read More
Tanzania Women Chamber of Commerce | 11-09-2022

ZIARA YA WANAWAKE NCHINI UTURUKI KUANZIA TAREHE 11-19 OKTOBA, 2022

Read More