Dar es salaam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindi Dkt. Husein Ally Mwinyi ameupongeza uongozi wa Chama cha Wanawake Tanzania (TWCC) kwa hatua kubwa waliopiga kwa jitihada kubwa wanazofanya katika kuwasaidia wanawake wafanyabiashara hapa nchini.
Rais Mwinyi ametoa pongezi hizo Julai 3,2022 alipofanya ziara katika Banda la Taasisi hiyo kujionea bidhaa mbalimbali za wajasiriamali waliopo chini ya TWCC katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kenye viwanja vya Mwalimu Juliua Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mwnyi alifika kwenye Maonesho hayo majira ya saa kumi za jionina kupokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TATRADE waandaji wa Maonesho hayo ambapo pamoja na mambo mengi alipata fursa ya kufanya ziara fupi ya kutembelea Mabanda mbalimbali na kujionea kazi mbalimbali za wafanyabiasha.
Akiwa TWCC Rais Mwinyi alipokewa kwa shangwe na sauti zikisikika za wajasiriamali hao kuimba wimbo wa 'Baba Baba' ikiwa ni ishara ya kumkaribisha huku Mwenyekiti wa TWCC Taifa na kurugezi Mtendaji wa Taasisi hiyo Mwajuma hamza wakimpitisha kwa wajasiriamali kuona kazi zao huku wajasiriamali hao wakiendelea kumimba na kumpigia makofi.
Kwa upande wake Mweyekiti wa TWCC Mercy Silla amemshukuru Rais Mwinyi kwa kuwatembelea na kwamba ujio wake umeamsha hari kwa wajasiriamali wao na kufarijika.
Credit
https://greenwavesmedia.blogspot.com