Programu ya Bid for Success (B4S) kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu kwenye manunuzi ya umma inarejea tena! Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) kinayo furaha kutangaza awamu ya nne ya mafunzo maalum kwa vijana kutoka Dar es Salaam na mikoa ya yote Tanzania.
Mafunzo haya yanalenga kuwapatia washiriki ujuzi na maarifa muhimu ili waweze kushiriki kwa ufanisi katika mchakato wa manunuzi ya umma. Usikose fursa hii adhimu ya kuboresha uwezo wako kupitia programu ya B4S!
šMAFUNZO YATAFANYIKA MKOA WA DAR ES SALAAM
Lengo la Mafunzo
ā¶ļøKuwajengea uwezo vijana kupanua wigo wa soko kupitia tenda za serikali na sekta binafsi.
ā¶ļøKuongeza ushiriki wa vijana kwenye Fursa za manunuzi ya Umma
ā
Vigezo vya kushiriki
1. Biashara yako iwe imesajiliwa ( uwe na TIN, na Leseni ya Biashara)
2. Biashara iwe inamilikiwa na kijana kwa asilimia 51 au zaidi
3. Biashara ilio tayari kukua na yenye mipango thabiti
4. ā Mjasiriamali au kampuni ambayo ina nia ya dhati ya kushiriki fursa za manunuzi ya umma kwenye Taasisi za serikali na kwenye sekta binafsi.
ā
Faida ya Kushiriki
1. Kupata elimu ya kina na ya kitaalam kuhusu masuala ya tenda na michakato ya kushiriki manunuzi ya umma
2. ā kufahamishwa kuhusu fursa mbalimbali za zabuni
3. ā kujengewa uwezo wa kukuza na kumiliki biashara endelevu
4. ā Kuunganishwa, kuwezeshwa na kusajiliwa kwenye mifumo ya kidigitali kwa ajili ya kuona fursa mbalimbali za tenda zinazotangazwa ukiwemo mfumo wa serikali wa manunuzi ya Umma (NeST), mifumo ya UN, Sekta binafsi. N.k
5 Kuweza kuunganishwa na Mlezi mtaalamu/Mentors atakaekuongoza kwenye mchakato wako wa kushiriki fursa za zabuni
6. ā Fursa ya kuongozwa kuweza kuandaa mpango biashara
7. ā Kusaidiwa kutengeneza profile nzuri ya kampuni
8. Kuunganishwa na taasisi za fedha pale unaposhinda tenda ili kuweza kutoa huduma husika
Mwisho wa kutuma Maombi kwa washiriki wa awamu ya NNE ni tarehe 31 January, 2025
Ili kuweza kushiriki, Jaza fomu hii https://forms.gle/eTajuaAfReMoDYN38
RAIS MWINYI AWAPONGEZA WAJASIRIAMALI WA TWCC
Read MoreTWCC WOMEN IN BUSINESS BREAKFAST MEETING 10 SEPTEMBA 2022
Read MoreZIARA YA WANAWAKE NCHINI UTURUKI KUANZIA TAREHE 11-19 OKTOBA, 2022
Read More