Tanzania Women Chamber of Commerce

PROGRAMU YA KUWEZESHA WANAWAKE NA VIJANA KUSHIRIKI MANUNUZI YA UMMA: BID FOR SUCCESS (B4S) - AWAMU YA NNE

Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) kinayo furaha kutangaza awamu ya nne ya Bid for Success (B4S), programu ya kipekee inayolenga kuwawezesha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika mchakato wa manunuzi ya umma. Programu hii maalum itafanyika katika Mkoa wa Mbeya, ikilenga mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Kuhusu Mafunzo ya B4S

Programu ya B4S inalenga kuwapatia washiriki maarifa na ujuzi muhimu ili kushiriki kwa ufanisi katika zabuni na tenda za serikali na sekta binafsi. Hii ni fursa adhimu ya kujijengea uwezo wa kukuza biashara yako na kushiriki katika soko pana.

Malengo ya Mafunzo

  • Kuwajengea uwezo wanawake na vijana kupanua wigo wa masoko kupitia tenda za serikali na sekta binafsi.
  • Kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika manunuzi ya umma na sekta binafsi.

Vigezo vya Kushiriki

  1. Biashara iwe imesajiliwa (uwe na TIN na leseni ya biashara).
  2. Biashara inamilikiwa na mwanamke au kijana kwa angalau asilimia 51.
  3. Biashara iliyo tayari kukua na yenye mipango thabiti ya maendeleo.
  4. Mjasiriamali au kampuni inayolenga kushiriki katika manunuzi ya umma na sekta binafsi.

Faida za Kushiriki

  • Kupata elimu ya kitaalamu kuhusu michakato ya tenda na zabuni.
  • Kufahamishwa kuhusu fursa za zabuni za serikali, sekta binafsi, na mifumo ya kimataifa kama NeST na UN.
  • Kujengewa uwezo wa kukuza biashara na kuunganishwa na taasisi za fedha.
  • Kupata usaidizi wa kuunda mpango wa biashara na wasifu bora wa kampuni.
  • Kuunganishwa na wakufunzi na miongozi ya kitaalamu (mentors) kwa ajili ya mafanikio ya zabuni.

Mwisho wa kufanya Maombi

Mwisho wa kutuma maombi kwa awamu ya nne ni Disemba 30, 2024.

Jinsi ya Kushiriki

Wajisajili wanahimizwa kujaza fomu kupitia kiungo hiki:
https://forms.gle/5uCBhSjq478r4fnHA

Usikose nafasi hii ya kipekee ya kuboresha biashara yako na kufungua milango mipya ya fursa!

Related Articles

Tanzania Women Chamber of Commerce | 12-07-2022

RAIS MWINYI AWAPONGEZA WAJASIRIAMALI WA TWCC

Read More
Tanzania Women Chamber of Commerce | 11-09-2022

TWCC WOMEN IN BUSINESS BREAKFAST MEETING 10 SEPTEMBA 2022

Read More
Tanzania Women Chamber of Commerce | 11-09-2022

ZIARA YA WANAWAKE NCHINI UTURUKI KUANZIA TAREHE 11-19 OKTOBA, 2022

Read More