Tanzania News

MWALIKO WA KUSHIRIKI MKUTANO WA UJUMUISHAJI WA KIFEDHA KWA WANAWAKE NA VIJANA 2024!

Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania(TWCC) inawakaribisha wanawake na vijana wajasiriamali pamoja na wadau mbalimbali kushiriki katika Women and Youth Financial Inclusion Summit tarehe 11 Desemba 2024 šŸ“…, katika JNICC, Dar es Salaam.

Huu ni mkutano wa kipekee utakaowawezesha washiriki kupata maarifa, fursa za mitaji, na ushirikiano mpya kwa ajili ya kukuza biashara na kufanikisha ujumuishaji wa kifedha kwa wanawake na vijana.

šŸŒŸ Kauli mbiu: Upatikanaji wa Huduma Nafuu za Kifedha kwa Wote

Faida za Kushiriki:
āœ… Kupata taarifa za kina kuhusu huduma za kifedha zinazolenga wanawake na vijana
āœ… Kushuhudia uzinduzi wa Mwongozo wa upatikanaji wa rasilimali fedha kwa wanawake na vijana
āœ… Kujifunza kuhusu fursa za mitaji wezeshi zilizopo
āœ… Kuunganishwa na wadau muhimu kutoka sekta za kifedha, biashara, na uwekezaji
āœ… Kupata nafasi ya kutoa maoni kuhusu jinsi ya kuboresha huduma za kifedha za kidigitali
āœ… Networking na washiriki zaidi ya 1,000 kutoka sekta mbalimbali
āœ… Kupokea nakala ya Mwongozo wa huduma za kifedha kwa wajasiriamali

šŸ‘‰ Usikose nafasi hii ya kipekee! Jisajili sasa bure kupitia kiunganishi hiki:
https://forms.gle/i1JY99j4My2DinGW6

šŸ“ Mahali: Julius Nyerere International Convention Centre
ā° Muda: Saa 2 asubuhi - 11 jioni
šŸ“ž Kwa mawasiliano zaidi: 0757 823 982

NB: Chakula na vinywaji vitapatikana!

Jiunge nasi kwenye safari ya kujenga msingi imara wa mafanikio ya kifedha na kibiashara. Usikose, nafasi ni yako! šŸŒŸ

#TWCC #FinancialInclusion #EmpoweringWomen #YouthEntrepreneurship #Wajasiriamali #KongamanoKubwa

Related Articles

Tanzania News | 07-02-2022

DC Jokate Mwegelo Azindua Rasmi Tuzo Za Wajasiriamali Wa Twcc Jijini Dar

Read More
Tanzania News | 07-02-2022

Taarifa Kwa Mawakala Na Waagizaji Wa Bidhaa Za Chakula Na Vipodozi Nje Ya Nchi

Read More
Tanzania News | 07-02-2022

Waziri Bashe Atangaza Sikukuu Ya Wakulima Nane Nane Kufanyika Mwaka Huu Wa 2022

Read More