TIN (Taxpayer Identification Number) ni namba ya kipekee inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kutambulisha mlipakodi katika shughuli zote za kibiashara na kodi. Hii ni muhimu kwa wafanyabiashara nchini Tanzania, kwani inarahisisha kupata leseni, kusajili magari, na kufanya mikataba mbalimbali.
UMUHIMU WA TIN YA BIASHARA:
1. Kusajili Biashara:Inahitajika kisheria kwa usajili rasmi wa biashara.
2. Kupata Leseni:TIN ni lazima kwa leseni za biashara na viwanda.
3. Ulipaji Kodi: TIN inatumiwa katika kulipa kodi kama VAT na Kodi ya Mapato.
Hatua za Kupata TIN kwa njia ya mtandao:
1. Kuandaa Mahitaji Muhimu:
- Kitambulisho cha Taifa (kadi ya kupigia kura, pasipoti, au uraia).
- Barua ya Makazi, Picha za Pasipoti, na Mkataba wa Pango (ikiwa ni eneo la kupangisha).
2. Usajili Mtandaoni:
- Tembelea link hii https://taxpayerportal.tra.go.tz/#/self-service/taxpayer-identity-number-registration kwenye tovuti ya TRA,kisha jaza fomu kwa usahihi na pakia nyaraka zako.
-Jaza fomu ya maombi: Jaza fomu ya maombi ya TIN kwa usahihi na ukamilifu. Hakikisha unaingiza taarifa sahihi, kwani taarifa hizi zitatumika kwa shughuli zako zote za kibiashara na kodi.
-Pakia nyaraka: Pakia nyaraka zote zinatohitajika kwenye mfumo. Hakikisha nyaraka hizo ziko katika ubora unaotakiwa na zinaonekeana vizuri.
Tuma maombi: Baada ya kukamilisha hatua zote, tuma maombi yako ya TIN
3. Alama za Vidole (Biometric):
- Nenda ofisi ya TRA iliyo karibu nawe kwa ajili ya alama za vidole ili kuthibitisha maombi yako.
4. Kupokea TIN:
- Ukikamilisha hatua zote, TRA itakutumia cheti cha TIN kwa barua pepe.
Tahadhari Muhimu:
Hakuna malipo kwa TIN, hivyo epuka vishawishi vya udanganyifu. Mara baada ya kupokea, hifadhi cheti chako kwa usalama.
DC Jokate Mwegelo Azindua Rasmi Tuzo Za Wajasiriamali Wa Twcc Jijini Dar
Read MoreTaarifa Kwa Mawakala Na Waagizaji Wa Bidhaa Za Chakula Na Vipodozi Nje Ya Nchi
Read MoreWaziri Bashe Atangaza Sikukuu Ya Wakulima Nane Nane Kufanyika Mwaka Huu Wa 2022
Read More