Benki ya NMB Plc. (“NMB”) ni benki ya biashara iliyosajiliwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kupitia vitengo vyake vitatu vya biashara: Rejareja, Jumla na Hazina, NMB inatoa huduma mbalimbali za kifedha na bidhaa kwa wateja wa reja reja, wakulima, wafanyabiashara wadogo na wakati, makampuni binafsi, Taasisi na Serikali. Benki ina matawi 226, Wakala zaidi ya 9,000 na ATM zaidi ya 700 nchini kote na inawakilishwa katika wilaya zote za Tanzania.NMB ina zaidi ya wateja milioni 4.