UTT AMIS ni kampuni ya uwekezaji yenye kuhusika na uanzishaji na uendeshaji wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja.Kampuni hii pia inatoa huduma za usimamizi wa amana(Wealth Management Services) UTT AMIS inafanya kazi zake kutokana na sheria za masoko ya mitaji na dhamana ya mwaka 1994(iliyorekebishwa) na kanuni ya Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja ya mwaka 1997. UTT AMIS kwa sasa inasimamia mifuko mitano ya uwekezaji ambayo ni Umoja, Wekeza Maisha, Watoto,kujikimu na Ukwasi.