Usajili wa Jina la Jipya la Biashara Kwenye mfumo wa Brela
Description
Vigezo vya Msingi: Lazima uwe na Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN) kutoka NIDA. Mmiliki wa jina la biashara lazima awe na NIN kutoka NIDA. Hatua za Usajili: Tembelea tovuti ya BRELA (www.brela.go.tz) au Mfumo wa ORS (https://ors.brela.go.tz/ors). Jisajili au ingia kwenye akaunti ya ORS. Chagua "Usajili wa Jina Jipya la Biashara" na ufuate hatua zinazohitajika. Jaza fomu ya usajili kwa taarifa zote muhimu na hifadhi kila hatua. Ongeza taarifa za mmiliki, ofisi, shughuli za biashara, na akaunti ya benki. Pakua na kusaini “Consolidated Form,” kisha ipakishe baada ya kuiscan. Fanya malipo kulingana na maelekezo, na maombi yako yatatumwa kwa BRELA kwa uchakataji. Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti ya BRELA.
Requirements
- Barua ya utambulisho kutoka sido
Online Application : No
Application Url : https://ors.brela.go.tz/ors
Cost : 0
Time Frame : siku 1
Payment Process :
Malipo kwa njia ya mitandao ya simu na benki kwa kutumia nambari ya malipo(control number)